Ripoti ya ABNA- Mjumbe wa Syria kwenye Umoja wa Mataifa Bashar Ja'afari amekamilisha hatua hiyo mapema huko Damascus katika jitihada za kuifanya Mashariki ya kati kutokuwa na silaha za maangamizi, ikiwemo kumaliza silaha za nyuklia zinazodaiwa kuwepo nchini Iran. Msemaji wa wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kwenye taarifa kwamba katibu mkuu amepokea barua kutoka Damascus, inayomuarifu kwamba rais Bashar Al-Assad amesaini amri ya kisheria ili Syria iweze kujiunga na mkataba huo na kuweza kuzuia uendelezaji, uzalishaji, kuhifadhi na kutumia silaha za kemikali pamoja na kuteketeza silaha hizi.
Bw. Ban Ki-moon amekaribisha maendeleo hayo, akisema ikiwa ni sehemu ya kuhifadhia mkataba, ametaka Syria ikubaliwe kwenye mkataba huo wa silaha za kemikali.